Jumatatu 21 Aprili 2025 - 14:42
Papa Fransisko Aaga Dunia

Vatikani imetangaza kuwa: Papa Fransisko, kiongozi wa Wakatoliki duniani, amefariki dunia tarehe 21 Aprili 2025, sawa na tarehe 1 Shahrivar 1404, akiwa na umri wa miaka 88 mjini Roma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawzah kutoka Tehran, Vatikani imetangaza kuwa Papa Fransisko, kiongozi wa Kanisa Katoliki, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 huko Casa Santa Marta mjini Roma. Papa Fransisko, ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, alikuwa akitoa huduma kama Papa wa 266 tangia mwaka 2013.

Yeye alikuwa Papa wa kwanza kutoka Bara la Amerika, mwanachama wa kwanza wa dhehebu la Jesuit, na pia ndie Papa wa kwanza ambae hakutoka barani Ulaya tangia Papa Gregori wa Tatu mnamo karne ya nane.

Bergoglio alizaliwa tarehe 17 Desemba 1936 huko Buenos Aires, Argentina, katika familia ambayo asili ya familia hiyo ni Italia. Kabla ya kuwa Papa, mnamo mwaka 1998 alikuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires na hatimae mwaka 2001 aliteuliwa na Papa Yohane Paulo wa Pili kuwa Kardinali.
Papa Fransisko alijulikana kutokana  na maisha yake yaliyo jaa unyenyekevu, msisitizo juu ya uadilifu katika jamii, na kuwatetea maskini. Papa huyo Badala ya kuishi katika kasri la Kipapa, alichagua kuishi katika nyumba ya kawaida ndani ya Vatikani, na mara nyingi alikuwa akitumia usafiri wa umma nchini Argentina.

Papa Fransisko alikumbana na changamoto mbali mbali kama vile, kashfa za kimaadili ndani ya Kanisa, na mnamo mwaka 2019 aliongoza mkutano wa kimataifa kwa ajili kushughulikia unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na makasisi.
Mwaka 2023, yeye ndiye aliyesimamia mazishi ya Papa Benedikto wa kumi na sita, na hivyo kuwa Papa wa kwanza kuongoza mazishi ya mtangulizi wake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha